Ufunuo wa Mbinguni na Kuzimu Kwa vijana 7 wa Kikolombia
Kwa pamoja kama kundi, vijana hawa 7 wa Kikolombia walichukuliwa na Yesu Kristo na kuonyeshwa Mbinguni na Kuzimu. Sikiliza masimulizi yao juu ya utukufu wa Mbinguni na ubaya wa Kuzimu. Imetafsiriwa na Mch.Peter John Mlay. www.spiritlessons.com |
Ufunuo wa Kuzimu
--- (Ushuhuda wa Kwanza
1) ---
Akasema palikuwa na mtu mmoja tajiri,
aliye vaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa
hanasa na masikini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake,
anavidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyo
anaguka kwenye meza ya yule tajiri,hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
Ikawa yule masikini alikufa,
akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa,
akazikwa. Basi kule Kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso,
akamwona Ibrahimu kwa Mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia akasema Ee baba
Ibrahimu, nihurumie, uumtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,
auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu
akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika
maisha yako na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa,
na wewe una umizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa
shimo kubwa,ili wale watakao kutoka huku, kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa
kwenu wasivuke kuja kwetu.
Bibilia,neno la Mungu
lipo wazi sana juu ya somo la Mbinguni na Kuzimu. Kwenye eneo hili ambalo
tumelisoma, Bwana anatuelezea juu ya maeneo mawili: Mbinguni na Kuzimu, hukumu
au wokovu. Hakuna eneo nje ya haya. Hakuna Pagatori. Hakuna Limbo,eneo ambalo
eti watu hufikia kwa muda halafu baadaye waende Mbinguni; Bibilia ipo wazi sana
juu ya hili.
(Aprili 11
1995)
Mungu alitupa ufunuo a
mbao ungebadili maisha yetu yote. Ni mara tuu tulikuwa tumeanza kufahamu juu ya
Mungu na juu ya neno lake.Sisi ni vijana saba ambao Munguametupa upendeleo na
jukumu kubwa la kuushirikisha ulimwengu ushuhuda huu.
Kila kitu kilianza majira
kama ya saa nne asubuhi 4.00 Tulikuwa tunaomba na tulikuwa tuna jiandaa
kwenda pikiniki baadaye siku ile . Ghafla majira ya saa nne 4.00 asubuhi nguvu
kuu ya mwanga mweupe uliangaza kupitia dirisha mojawapo. Wakati mwanga
ulipotokea, sisi sote kwa haraka tulianza kuongea kwa lugha mpya na tulibatizwa
na Roho Mtakatifu .
Kwenye muda ule, sisis
sote tulishangazwa na kuogopeshwa na kile tulicho kiona. Mwanga ule wa utukufu
ulikuwa ukiimulika chumba chote. Mwanha huu ulikuwa na nguvu kuliko mwanga wa
jua. Katikakati ya ule mwanga, tuliwaona malaika wengi wakiwa wamevaa mavazi
meupe. Malaika hawa walikuwa ni wazuri sana, warefu, na wenye mvuto wa sura.
Kari kati ya Malaika wale
tuliona kitu cha kutushangaza --umbo la mwanadamu. Umbo hili lilikuw ni
la kiumbe maalumu sana, mtu aliye kuwa amevaa nguo nyeupe sana Nywele
zake ni kama nyuzi za dhahabu. Hatukuweza kuuona uso wake kwa sababu ulikuwa
unang,aa sana. Hata hivyo tuliweza kuuona mshipi wa dhahabu ukiwa matiti mwake,
na maandishi ya dhahabu yaliyosema: "Mfalme
wa wafalme na Bwana wa mabwana ." Alikuwa amevaa viatu
vya dhahabu halisi miguuni mwake, na uzuri wake haukuwa na mfano.Tulipo uona
uwepo wa mtu huyu wote kwa pamoja tulisujudu kwa kupiga magoti.
Baadaye tulianza kuisikia
sauti yake.Ilikuwa ni ya kipekee na ya ajabu sana;kila neno liliingia
miyoyonimwetu kama vile upanga ukatao kuwili; kama vile ilivyo andikwa katika
neno la Mungu(Waebrania 4:12). Alizungumza nasi
kwa wepes lakini kwa maneno yenye nguvu sana. Tulisikia sauti yake ikisema nasi
kuwa, "Watoto wangu wadogo, msiogope,
mimi ni Yesu wa Nazarethi, na nimewatembelea kuwaonyesha mambo ya ajabu ili
muweze kuyaonyesha na kuyaelezea kwenye, Miji, Mataifa, majiji, makanisa na
kila mahali. Pale nitakapo waambia mwende, mtaenda, na pale nitakapo waambia
msiende msiende."
Bibilia takatifu, neno la
Mungu, linasema katika Yoeli 2:28 "Hata itakuwa baaada ya hayo ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya
wote wenye mwili; na wana wenu waume na wake watatabiri ,wazee wenu wataota
ndoto, na vijana wenu wataona maono." Huu ni wakati ambao
Bwana anauandaa kwa kila mmoja.
Baadaye kitu kigeni
kilitokea, mwamba ulitokea katikati ya kile chumba, na Bwana ambaye tulikuwa
pamoja naye, alitufanya kuingia ndani ya ule mwamba.Mwamba ule ulikuwa na urefu
wa karibu inchi saba hivi juu ya sakafu, na shimo kubwa lilitokea pale
sakafuni.Lilikuwa ni kubwa,jeusi,mwanya au uwazi wa kutisha.Kwa haraka tuliweza
kuwa juu ya ule mwamba na kuzama chini kupitia ule uwazi sakafuni.Ilikuwa ni
giza nailituongoza hadi katikati ya dunia.
Wakati tulipo kuwa ndani
ya giza lile baya, tuliogopa sana!tulitishika sana kiasi kwamba tulimwambia
Bwana, "Bwana hatutaki kwenda eneo lile! Usitupeleke eneo lile
Bwana! Tutoe mbali na eneo hili Bwana!" Bwana alitujibu
kwa sauti nzuri na ya huruma, "Uzoefu huu
ni wa muhimu sana ili muweze kuuona na kuwaelezea wengine."
Tulikuwa kwenye tanuru
lenye sura kama ya pembe, na tulizubaa kwa kuangalia vivuli, mapepo na maumbo
yalikuwa yakihama toka eneo moja kwenda jingine. Tuliendelea kwenda chini na
chini zaidi.Ndani ya sekunde chache tulikuwa tukijisikia watupu na uoga mwingi.
Baadaye tulifika kwenye
baadhi ya mapango makubwa;kwenye malango ya kutisha, kama vile njia
panda. Hatukutaka kuingia mle ndani.Tuligundua harufu ya kutisha na joto
lilotutetemesha.Mara tulipoingia tuliona vitu vya ajabu na maumbo ya kutisha.
Eneo lote lilikuwa limezungukwa na miali ya moto;na katikati ya ile mioto,
kulikuwepo miili ya watu maelfu. Walikuwa wakiteseka katika mateso makuu.Eneo
lilikuwa ni la kuogopesha sana, hatukutaka kuona kile tulichokuwa tunaonyeshwa.
Eneo hili lilikuwa
limegawanyika katika maeneo tofauti ya mateso na maumivu.Moja ya eneo la
kwanza ambalo Bwana alituruhusu kuliona ni "Bonde la sufuria la
kupikia" kama tulivyoliita. Kulikuwa na masufuria
mamilioni.Masufuria haya yalikuwa yamelazwa usawa wa aridhi; kila moja lilikuwa
linatokota uji wa moto.Ndani ya kila moja ilikuwepo roho ya mtu aliyekuwa
amekufa na kwenda kuzimu.
Mara tuu zile roho zilipo
mwona Bwana, zilianza kupiga kelele na kulalamika, "Bwana, utuhurumie!
Bwana nipe nafasi ya kutoka nje ya eneo hili! Bwana, nitoe nje na
nitauambia ulimwengu kwamba eneo hili ni la kwecli!" Lakini
Bwana hata hakuwatazama. Walikuwepo mamilioni ya wanaume kwa wanawake na
vujana eneo lile. Pia tuliwaona watu wandoa ya jinsia moja na walevi
kwenye mateso.Tuliwaona watu hawa wote wakipiga makelele kwa maumivu.
Ilituogopesha kuona jinsi
ambavyo miili yao ilikuwa imeharibiwa. Minyoo ilikuwa inaingia na kutoka
kupitia kwenye mafuvu ya macho yao, ya midomo yao, na masikio; na ilikuwa
ikijiingiza kwenye ngozi kuingia miilini mwao. Hii inatimiza neno la Mungu
lililo andikwa kwenye kitabu cha Isaya 66:24 "Nao watatoka nje na kuitizama mizoga ya watu walioniasi;
maana funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika; nao watakuwa chukizo
machoni pa wote wenye mwili." Pia katika Marko 9:44,"Ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki."
Tulikuwa tumeogopeshwa na kile tulicho kuwa tunakiona. Tuliona miali ya moto
kama ya urefu wa inchi 9 mpaka 12 hivi. Ndani ya kila mwali wa moto
kulikuwepo na roho ya mtu aliye kufa na kwenda kuzimu.
Bwana alituruhusu kumwona mtu
ambaye alikuwepo ndani ya mojawapo ya masufuria yale ya moto. Alikuwa kichwa
chini miguu juu na nyama za uso wake zilikuwa ziki anguka chini kwa vipande.
Alibaki akimwangalia Bwana kwa makini; na baadaye alianza kupiga makelele na
kuliitia jina la Yesu. Alisema, "Bwana nihurumie! Bwana nipe
nafasi! Bwana nitoe nje ya eneo hili!" Lakini Bwana Yesu
hakutaka kumwangalia.Yesu alimgeuzia mgongo wake. Wakati Yesu alipo fanya
hivyo, mtu yule alianza kulaani na kumtukana Bwana. Mtu huyu ni
John Lennon, mjumbe wa shetani wa kundi la mziki la "The
Beatles." John Lennon alikuwa ni mtu aliyefanya mizaha na kumtania
Bwana wakati wa maisha yake.Alisema kuwa Ukristo ungekwenda kutokomea na Yesu
Kristo angesahaulika na kila mmoja.Hata hivyo leo, mtu huyu yupo kuzimu na Yesu
Kristo yuu hai!! Ukristo pia hauja tokomea.
Tulipo anza kutembea
kwenye ukingo wa eneo hili, roho zilikuwa zikinyoosha mikono yao kwetu na
kutaka rehema.Walimwomba Yesu kuwaondoa ndani ya eneo lile, lakini Bwana hata
hakuwaangalia.
Baadaye tulianza kwenda
katika maeneo tofauti tofauti. Tulifika katika eneo lenye kutisha zaidi
kuzimu,mahali ambapo mateso makubwa sana hufanyika; katikati ya kuzimu. Eneo
lenye mchanganyiko mkubwa sana wa mateso;mateso ambayo mwanadamu yeyote hawezi
kamwe kuyaelezea. Watu pekee hapa ni wale tuu ambao walimjua Yesu na neno
la Mungu. Walikuwepo wachungaji,wainjilisti,wamisionari na aina zote za watu
ambao waliwahi kumkubali Yesu na kuujua ukweli;lakini waliishi maisha ya pande
mbili.
Walikuwepo pia wale waliorudi
nyuma kiimanin; mateso yao yalikuwa ni makubwa mara elfu zaidi ya
wengine. Walikuwa wakipiga makelele na kuomba rehema kwa Bwana, lakini
neno la Bwana linassema katika kitabu chaWaebrania 10:26-27, "Maana kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea
ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia
hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao."
Roho zile zilikuwepo pale
kwa sababu zilihubiri,zilifunga , ziliimba,na kuinua mikono yao kanisani lakini
mitaani na majumbani walikuwwepo katika uasherati, uzinzi, uongo,
unyanganyi. Hatuwezi kumdanganya Mungu. Bibilia inasema kwake ambaye
alipewa vingi, atadaiwa vingi. (Luka 12:48)
Mungu baadaye alituruhusu
kuwaona wanawake wawili ambao walikuwa ni wakristo wakiwa duniani, lakini
hawakuwahi kuishi maisha ya haki mbele za Bwana Mmoja akamwambia mwenzake,
"Wewe masikini mlaaniwa! ni makosa yako kwamba nipo eneo hili!
hukunihubiria Injili takatifu! na kwasababu hukuniambia ukweli, nipo sasa hapa
kuzimu!" Walisema maneno haya katikati ya miali ya moto, na
walichukiana kwasababu hakuna upendo,rehema wala kusameheana kuzimu.
Kulikuwa na roho maelfu
ya wale ambao waliwahi kulijua neno la Mungu, lakini maisha yao hayakuwa safi
mbele ya uwepo mtakatifu wa Bwana. "Huwezi
kucheza na Mungu wala na miali ya moto wa kuzimu!" Bwana
alisema. Pia alituambia, "Wana
wangu, mateso yote duniani kwa pamoja sii kitu,SII
KITU, kulinganisha na mateso yale mtu hupata katika eneo lile zuri la kuzimu."
Kama ni hatari kiasi hicho kwa yule anayeteseka kidogo kuzimu, ni mbaya kiasi
gani basi kwa yule aliyeko katikati ya kuzimu ? ambao waliwahi kulijua neno la
Bwana na kwenda mbali nalo. Baadaye Bwana alituambia kuwa wale wanao weza
kucheza na moto duniani sii hivyo kuzimu hawawezi kamwe.
Tuliendelea kutembea
maeneo tofauti tofauti na Bwana alituonyesha watu wa aina mbali mbali. Tuliweza
kuona kuwa watu wote pale walikuwa na aina kama sita za mateso.
Kulikuwepo na roho zilizo teswa na mapepo kwa aina zote za adhabu. Aina
nyingine ni ufahamu wao uliosema, "Kumbuka wakati walipo kuhubiria,
kumbuka wakati ulipo sikia neno la Mungu, kumbuka walipo kuambia habari za
kuzimu na ulicheka juu ya hilo !" Ufahamu wao wenyewe uliwatesa;
kama vile minyoo ile iliyopita juu ya miili yao, kama vile moto ule ulao ambao
ni mkali mara elfu, elfu zaidi ya tunavyojua.Hii ni zawadi ambayo shetani anayo
kwa wote wanao mtafuta na kumfuata.
Neno la Bwana linasema
katika Ufunuo 21:8 "Bali waoga na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na
wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni
katika lile ziwa liwakao moto na kiberiti.Hii ndiyo mauti ya pili."
Baadaye Bwana
alituonyesha mtu aliyeua watu sita. Watu wale sita walikuwa wamemzunguka, na
walikuwa wakimpigia kelele wakisema, "Ni makosa yako kuwa tupo hapa
wote, MAKOSA YAKO!" Muuaji alijitahidi kufunika masikio yake
kwasababu hakutaka kuwasikiliza, lakini hakuweza kuepuka kusikia kwani kule
kuzimu fahau zako zinakuwa hai zaidi.
Roho mahali pale zilikuwa
zikiteseka kwa kiu ya maji isiyo vumilika na kutoshelezwa kwa njia yeyote;Kama
vile kwenye Bibilia habari za Lazaro na yule tajiri. (Luka 16:19) Tajiri kule kuzimu alitaka tuu
tone la maji, yangemtosha. Neno la Bwana linasema katika Isaya34:9, "Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake
yatageuzwa kuwa kiberiti, na aridhi yake itakuwa lami iwakayo."
Katika eneo lile,kila
roho ilikuwa katikati ya moto. Watu huona mfano wamaji ya mto safi katikati ya
moto na wanapo jaribu kuufikia, mito hiyo hugeuka kuwa moto.Huona pia miti
yenye matunda ambayo hutoa maji, lakini wanapo jaribu kuchukua, huungua mikono
yao na mapepo huwacheka.
Baadaye Mungu alituchukua
baya zaidi ya maeneo mengine ambayo tumewahi kuyaona. Tuliona ziwa la moto na
kemikali. Upande mmoja wa lile ziwa kulikuwepo na ziwa dogo zaidi. Ndani ya
ziwa lile dogo, kulikuwepo naroho, milioni, milioni, zikilia na kuomba kwa
Bwana kuwa rehemu. Walimwambia, "Bwana tafadhali!
Tutoe nje ya eneo hili hata kwa muda kidogo! Tafadhali nipe nafsi ya kwenda
nje!!!" Hatahivyo, Bwana hakuweza kufanya chochote kwa
sababu hukumu yao tayri ilisha pangwa.
Kati ya roho zile milioni
na milioni, Bwana alituruhusu kumwangalia mtu mmoja ambaye mwili wake nusu
ulikuwa umezama katika ziwa la moto.Bwana alituruhusu kuelewa na kuyafahamu
mawazo yake.Jina la mtu huyu ni Marko.Tulishangaa na yale mtu huyu aliyojisemea
mwenyewe katika mawazo yake. Tulijifunza somo ndani yetu tulipo yasikia
mawazo yake yafuatayo, "Ningetoa chochote kile kuwa katika nafasi yako
sasa! Ningetoa kitu chochote ili kwenda duniani kwa dakika moja tuu. Singejali
kama ningekuwa na hali mbaya, mgonjwa sana, ninayechukiwa sana, au mtu masikini
kuliko wote duniani, ningetoa chochote kuweza kwenda duniani! kwa dakika moja
tuu duniani." Bwana Yesu alikuwa ameushika mkono wangu. Yesu
aliyajibu mawazo ya Mariko kwa kusema, "Mariko,
kwanini ungependa kurudi duniani hata kwa dakika moja?"
Kwa kulia na kwa sauti ya mateso, alimwambia Yesu, "Bwana!
nitatoa kitu chochote kuweza kurudi duniani tuu kwa ajili ya kutubu na kuokoka."
Bwana aliposikia kile
ambacho Mariko alisema, niliona damuikitoka katika majeraha ya Yesu na machozi
yaliyajaza macho yake na alisema, "Mariko,
umechelewa sana! Minyoo imewekwa iwe kitanda chako na minyoo itakufunika."
(Isaya 14:11) Wakati Bwana alipo
mwambia hivyo, alizama kwenye ziwa lile mojakwa moja. Ni kwa huzuni kuwa roho
zile zote hazina tena tumaini. Ni sisi tuu tuliopo duniani ambao tunayo nafasi
ya kutubu leo na kwenda Mbinguni na Bwana wetu Yesu Kristo.
Nina kuacha sasa na dada
yangu kuendeleza ushuhuda huu, asante.
--- (Ushuhuda wa pili 2, Lupe) ---
Mungu awbariki kaka zangu wapendwa.Tusome neno la
Bwana kutoka Zaburi
18:9. "Aliziinamisha mbingu akashuka,
kukawa na giza
kuu chini ya miguu yake" Wakati Bwana alipo ifikia mikono
yangu, niliishika mikono yake tulianza kushuka chini kupitia tanuru lile.Tanuru
lilikuwa linazidi kuwa giza
na giza
kiasi kuwa sikuweza hata kuuona mkono wangu, ambao haukuwa umeushika mkono wa
Bwana
Ghafla, tulikipita kitu fulani cheusi na chenye kutoa
cheche; kilikuwa kikitoa sauti.Giza lilikuwa kuu sana, mikono yako isdinge weza hata kuguza
kuta za lilr tanuru.. Tulishuka kwa kasi sana,
kwamba nilisika kuwa roho yangu ilikuwa ikitengwa na mwili wangu.
Mara nilihisi
harufu mbaya ya kitu kilicho oza sana. Kama harufu ya miili iliyo
oza. Ilikuwa ikizidi kila mara. Baadaye nilisikia sauti za mamilioni na
mamilioni ya roho. Walikuwa bila kukoma wakipiga makelele, wakilia, na
kuhuzunika.Ilikuwa inaogopesha sana hivyo nilimgeukia Bwana na kumuuliza,
"Bwana , unatupeleka wapi? Bwana nirehemu! Tafadhali
nihurumie!" Bwana alisema tuu, "Ni muhimu kwamba uone hili, ili uweze kumwaambia
kila mmoja."
Tuliendelea chini kupitia tanuru
hili lenye sura ya pembe hata tulipo fika eneo ambalo lilikuwa ni giza tupu.
Kama vile kuondoa pazia zito machoni mwangu, baadaye niliona miali ya moto
milioni nba milioni.Kwa ubaya sana nilisikia sauti zile maumivu lakini sikuweza
kumwona yeyote. Niliogopa haswa. Nilimwambia Bwana, "Oh
tafadhali Bwana nirehemu!Ooh tafadhali Bwana unirehemu ! Usinipeleke eneo
hili! Nisamehe!" Katika muda huu, sikujua tuu kuwa mimi ni
mtazamaji tuu wa kuzimu, nilifikiri ilikuwa ni siku ya mwisho. Nikiwa
nimesimama mbele ya Bwana Yesu, nilikuwa nikitetemeka kwa nguvu kwa sababu
nilifikiria kuwa ilikuwa ni mwisho wa maisha yangu.
Tulisogea karibu katika
moto mkubwa mbele yetu; ulikuwa mkubwa na uliwaka kwa ukali. Niliendelea kwenda
chini taratibu, nikiona miali ya moto mingi na kusikia sauti za mamilioni ya
roho zilizo lia kwa sauti kwa pamoja.
Baadaye niliona meza ya
mti ambayo haikufikiwa na moto.Kulikuwa na kitu kama chupa za bia juu
yake.Zilionekana kama ni za kuburudisha lakini zilijaa moto ndani yake.Nilipo
kuwa ninaangalia, mtu alitokea kw ghafla.Mwili wake ni kama ulikuwa umekwisha
na kile kilichokuwa kimebaki ni vazi lililo jaa tope na moto. Alikuwa
amepoteza macho yake, mdomo, na kila unywele kule motoni. Aliweza kuniona bila
hata macho yake.. Nina kuambaia huyu ni mtu anaye waza , anayetafakari ,na
kuona kwa kweli; sii kwa mwili wako wa asili.
Mtu huyu aliunyosha mkono
wake kwa Bwana na kuanza kulia, akisema,, "Bwana nirehemu! Bwana
nirehemu! Nipo kwenye maumivu! Ninaunguzwa! Tafadhali
nirehemu na unitoe mahali hapa!" Bwana alimwangalia kwa
huruma,na nilianza kusikia kama joto kwenye mkonom wangu.Niliangalia na kuona
kuwa ni damu...damu ya Yesu! Damu ya Bwana ilitoka mkononi mwake alipo
kuwa akimwangalia mtu huyu akiteseka na kuzungukwa na moto
Baadaye mtu huyu aligeuka
na kuelekeza mawazo yake kwenye meza na kutembea kuelekea zile chupa.Alichukua
chupa na alipo kuwa karibu ya kuinywa, moto na moshi ulitoka ndani ya ile
chupa. Aligeuza kichwa chake tena na ulia kwa jinsi ambavyo sijawahi tena
kusikia..Alilia kwa maumivu makuu sana na masononeko na alianza kunywa kile
kilicho kuwepo ndani ya ile chupa.Lakini chupa ile ilijaa asidi\ tindikali na
koo lake liliaribiwa karibu na kwisha. Ungeweza kuona tindikali ile ikipita mle
tumboni na kumuumiza.
Namba ile 666 ilikuwa
imechimbiwa juu ya upaji wa uso wake. Juu ya kifua chake kulikuwepo na
sahani iliyo fanywa na malighafi isiyo julikana mabyo hata ule moto
wala minyoo isingeweza kuiangamiza. Ilikuwa na maandishi juu yake lakini
hatukuweza kuyaelewa Bwana kwa neeema yake kuu, alitupa tafsiri ya kile kilicho
kuwa kimeandikwa. "Nipo hapa kwa sababu mimi ni mlevi."
Alimwomba Bwana rehema,lakini neno la Mungu lipo wazi sana linaposema katika 1 Wakotintho 6:10 "Wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji,
wala wanyanganyi, hawatauridhi ufalme wa Mungu."
Mungu alinionyesha hali
ya mtu huyu muda mfupi kabla hajafaa duniani, kama vile sinema.Ilikuwa ni kama
TV kubwa ikinionyesha sekunde zake za mwisho kabla hajafa.Jina lake
aliitwa Luis na alikuwepo baa akinywa pombe. Niliona meza ileile na chupa
ileile pale baa.Kuizunguka meza ile walikuwepo marafiki zake. (Naweza
kukuambia jambo hili sasa kuwa yupo RAFIKI MMOJA TUU WA KWELI, na jina lake ni
YESU KRISTO.Yeye ni rafiki mwaminifu.) Luis alikuwa akinywa na
marafiki zake walikuwa tayari wamelewa. Rafiki yake mkubwa alichukua
chupa na kuipasua na kuanza kumpiga nayo Luis . Alipo onma Luis amelala chini
alikimbia,na Luis alitokwa na damu hadi kufa pale sakafuni. Jambo la huzuni
sana ni kuwa alikufa bila Bwana Yesu.
Katikati ya mambo haya
yote, kwa jinsi roho zile zote zilivyo kuwa zinalia, nilimuuliza Bwana, "Oh
Bwana, tafadhali niambie je mtu huyu alijua habari zako? Alifahamu habari
za wokovu wako?" Bwana kwa huzuni alijibu, "Ndiyo, Lupe, alijua habari zangu. Alinipokea kama Bwana
wake, lakini hakunitumikia." Baadaye nilijisiki uwoga
zaidi. Luis alilia kwa sauti na kupiga kelele"Bwana hii
inaumiza!inaumiza! tafadhali nirehemu!" Aliunyoosha mkono wake
tena kwa Bwana lakini Yesu aliuchukua mkono wangu na tulitembea kutoka eneo
lile la moto. Moto ulio muunguza Luis ulikuwa na ukali zaidi, na alilia kwa
sauti kuu zaidi, "Nirehemu! Nirehemu!!" Alitokomea
baadaye kwenye ule moto.
Tuliendelea kutembea,
eneo hili lilikuwa kubwa na la kuogopesha! Tuliufikia moto mwingine na
nimwambia Bwana, "Bwana, hapana.! Tafadhali sitaki kuona tena
haya! nakuomba unisamehe!Tafadhali nisamehe! sitaki kuona haya!"
Hivyo niliyafunga macho yangu,lakini haikusaidia, kufunga au kufungua bado
niliona kila kitu.Moto huu ulianza kwenda chini taratibu na baadaye nilimwona
mwanamke.Alikuwa amefunikwa na tope, na tope lilijaa minyoo mingi. Alikuwa bado
na nywele chache zilizo baki na alikuwa amezungukwa na minyoo pamoja na
tope. Alikuwa analiwa na ile minyoo kila eneo na alilia, "Bwana
nirehemu! Bwana nirehemu na unisamehe!niangalie.Hii inaumiza ! Nirehemu !
Niondolee hawa minyoo!Nitoe ndani ya mateso haya kwa sababu yananiumiza sana!"
Bwana alimwangalia tuu kwa huzuni kuu . Tukiwa tumeshika mikono yake tuliweza
kuhisi maumivu na huzuni ndani ya moyo wa Yesu, kwa roho zote zinazo
potea na kuchomwa milele motoni kuzimu.
Mwanamke hakuwa na macho
wala nyama midomoni, lakini aliweza kuona na kuhisi ; maumivu yote
yalikuwa ni makuu sana. Alikuwa na chupa mkononi mwake, iliyo jaa tindikali,
lakini aliamini kuwa ni manukato. Niliweza kuona kuwa ni tindikali na kila mara
alipo ipulizia mwilini mwake, ilikuwa ikimuunguza. Hata hivyo aliendelea
kuitumia ile tindikali tena na tena.Aliendelea kusema kuwa ile ni manukato ya
dhamani sana.Aliamini pia kuwa alikuwa amevaa nguo isiyo na shingo, lakini kile
nilicho kiona kiliwa ni nyoka iliyo mzingira shingoni. Aliamini kuwa
alikuwa amevaa ushanga wa kupendeza sana, lakini niliona zilikuwa ni minyoo
ya kweli kabisazenye urefu wa kam futi moja wakiwa na hasira na kujichimbia
ndani ya mifupa yake.Alikuwa amevaa chapa ya chuma ambayo kila mmoja anayo kule
kuzimu. Iliandikwa, "Nipo hapa kwa ajili ya wizi."
Mwanamke huyu hajutii
dhambi zake. Bwana alimuuliza, "Magdalena,
kwanini upo eneo hili,? Alijibu, "Haikunisumbua kuwaibia
wengine.Kile nilicho jali ni kupata vito vya dhamani na manukato za dhamani.
Sikujali ni nani niliye muibia, mradi tuu nipendeze."
Nili ushika mkono wa
Kristo nilipo ona minyoo ikimwingia mwilini mwake .Magdalena aligeuka akitafuta
kitu fulani. Nilimuuliza Bwana tena, "Bwana, je mtu huyu alikujua?"
Na Bwana alijibu, "Ndiyo, mtu huyu
alinijua."
Magdalena alianza
kuangalia pembeni, akisema, "Bwana, yupo wapi mwanamke yule amliye
ongea nami habari zako?Yupo wapi? Nimekuwepo hapa kuzimu kwa miaka 15 sasa."
Watu wote kuzimu wanaweza kukumbuka kila kitu. Mgadalena aliendelea kusema,
"Yupo wapi mwanamke huyu? Siwezi kumwona!" Nilijua
kuwa mwili wake usingeweza kugeuka kwasababu nyama za ule mwili zingebaki
mahali pamoja. Alijaribu kugeuka na kuangalia kwenye mioto mingine, kumtafuta
yule mwanamke aliye ongea naye juu ya Mungu. Bwana alisema, "Hapana! hapana, Magdalena, hayupo hapa. Yule
mwanamke aliye kuambia habari zangu yupo kwenye Ufalme wa Mbinguni pamoja nami."
Kwa kusikia hili,
alijitupa wmenyewe chini ya ule moto ambao ulimuunguza zaidi. Bango lake
lilikuwa likimhukumu kuwa ni mwizi. Nataka usome neno la Bwana katika Isaya 3:24. "Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa
uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizo sukwa vizuri,
upaa; badala ya kisibau mavazi ya gunia, na kutiwa alama mwilini kwa moto
badala ya uzuri."
Kwa jinsi tulivyo endelea
kutembea na Bwana, niliona eneo la miraba lililojaa minyoo.Kulizunguka
kulikuwepo na chuma chenye moto mwekundu.Kwenye eneo lile la miraba kulikuwepo
na ubao ulio angaza kila mahali . Ubao uliandikwa,"Karibuni
waongo na wasengenyaji." Mwisho wake kulikuwa na ziwa linalo
tokota. Ilikuwa ni kama uji wa kikemikali unao tokota. Baadaye
niliwaona watu walio uchi kabisa wakija chini eneo lile. Walipo kuwa wanateleza
kuja ngozi zao zilikuwa zinabaki kwenye kile chombo.Walipo angukia kwenye ziwa
lile, ndimi zao zilitanuka hadi kupasuka na minyoo ilitokea badala ya ndimi
zile..Matezo yao yalianza. Neno la Mungu linasema katika Zaburi 73:18-19 "Hakika wewe huwaweka kwenye utelezi, Huwaangusha
mpaka palipo haribika. Namna gani ukiwa mara! wametokomea na kutoweshwa kwa
utisho."
Baada ya kuona hili,
tulichukuliwa tena , nje ya kuzimu. Nina taka kukuambia kuwa Mbingu na
Kuzimu ni za kweli kuzidi hata ulimwengu wetu huu tunao ujua. Ni hapa tuu
unapo weza kuamua ni upande upi unao taka kwenda; kuutumia umilele na Yesu au
kuunguzwa kuzimu.Bwana aliendelea kutuambia,"Pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye niona mimi, pasipo utakatifu
hakuna mtu atakaye niona mimi." (Waebrania 12:14) Hii ndiyo sababu
ninakuambia kitu kile kile sasa, "Pasipo utakatifu hakuna mtu
atakaye mwona Bwana."
--- (Ushuhuda wa tatu 3, Sandra) ---
Hebu twende pamoja kwenye neno la Bwana katika Mathayo
10:28 " Msiwaogope wauao mwili,
wasiweze kuiua roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho
pia katika Jehanum."
Wakati roho inapo fika kuzimu, mtu huyo huchukua mwili
wa mauti.Bwana Yesu alinishika mkono wangu na tulianza kwenda chini kupitia
tanuru lenye giza
kuu linaongoza kwenda katikati ya dunia. Tulifika eneo lenye milango mingi;
mmoja wao ulifunguka na tuliingia pamoja na Bwana. Sikuweza kuuachia mkono wa
Bwana maana nilijua kwa kufanya hivyo ningelibakia mle kuzimu milele.
Baada ya kuingia mlango ule, niliona ukuta mkubwa
sana.Kulikuwa na watu kwa maelfu waliokuwa wametundikwa vichwa vyao na komeo,
na pingu zilizo wafunga mikono yao
ukutani. Tuliona
pia maelfu ya watu wakiwa wamesimama katikati ya mioto kila eneo.
Tulikwenda mbele ya ile
mioto na mara ilianza kutulia taratibu.Mara niliweza kumwona mtu mle ndani, na
alipo ongea, niliweza kujua kuwa alikuwa ni mtu.Mtu huyu alikuwa amevaa vazi la
Kikuhani lililokuwa limeharibiwa kabisa .Minyoo ilikuwa ikimwingia na
kutoka.Alionekana mweuusi kutokana na kuunguzwa na moto. Macho yalikuwa
yamemtoka na nyama yake ilikuwa imeyeyuka na kuanguka chini. Lakini baada ya
nyama yote kuanguka chini baadaye humrudia na tendo hili huanza tena.
Alipo mwona Yesu,
alisema, "Bwana unirehemu,unirehemu! Tafadhali nitoe hapa hata kwa
kitambo kidogo tuu! kwa dakika tuu!" Kwenye kifua chake
lilikuwepo bango lilosomeka, "Nipo hapa kwa ajili ya wizi."
Wakati Yesu alipo kuja
karibu, alimuuliza yule mtu,"Jina lako
ni nani?" Akajibu, "Andrea, jina langu ni Andrea,
Bwana." Bwana akamuuliza, "Ni
kwa muda gani umekuwepo hapa?" Andrea alijibu, "Nimekuwepo
hapa kwa muda mrefu sana." Mtu huyu alianza kuelezea habari za
maisha yake. Alisema, alikuwa na kazi ya kukusanya fungu la kumi na
kupanga jinsi ya kugawa fedha za kanisa lake la Katoliki kwa masikini.Hata
hivyo,alikuwa akiiba zile fedha. Kwa macho yaliyo jaa huruma, Bwana alimuuliza,
"Andrea, Uliwahi kuisikia injili ?"
Andrea alijibu, "Ndio Bwana, alikuwepo mwanamke mmoja wa kikristo aliye
ingia kanisani na alihubiri injili mara moja, lakini sikutaka kuipokea.Sikutaka
kuiamini, lakini naiamini sasa! Sasa naamini kuwa huu ni ukweli! tafadhali
Bwana nitoe mahali hapa,hata kwa kitambo tuu!"
Alipo kuwa akiongea,
minyoo ilikuwa ikitambaa kwenye mafuvu ya macho yake yakitokea masikioni, na
kuingia tena kupitia mdomo wake. Alijaribu kuwavuta nje kwa mikono yake lakini
haikuwezekana. Alikuwa akipiga makelele kwa na kumwomba Mungu amrehemu.
Aliendelea kumwomba Yesu amtoe mahali pale. Mbaya zaidi kulikuwepo na pepo
linalo mtesa, muda wote yakimchoma na mikuki yao.Pepo hili lilifanana na midoli
ile tuliyo nayo hapa duniani tunayo iita "Joridano". Niliiona
midoli hiyo kuzimu, lakini sasa haikuwa tena ni midoli;yalikuwa hai na ni
mapepo. Yalikuwa ya urefu karibu futi tatu na meno makli sana. Damu zinawatoka
mdomoni na macho yao yalikuwa ni mekundu kabisa.
Yalikuwa
yakimsumbua Andrea kwa nguvu zao zote, pamoja na wengine walio
kuwepo eneo hili la kuzimu.. Nilipo ona hili, nilimuuliza Bwana inawezekana je
midoili ya duniani, kufanana kama yale mapepo.Bwana aliniambia kuwa yale ni
mapepo ya huzuni.
Tulipo endelea, tuliwaona
maelfu ya watu kwenye mateso,Wakati roho inapo mwona Bwana, zilijitahidi
kumfikia kwa mikono isiyo na ngozi.Nilimwona mwanamke aliye anza kupiga
makelele alipo mwona Bwana Yesu. Alilia, "Bwana tafadhali nirehemu!
nitoe mahali hapa!" Alikuwa akiteseka sana na aliunyoosha mkono
wake kwa Bwana.Aliendelea kumwomba Bwana amtoe eneo lile hata kwa sekundr
moja. Alikuwa yuu uchi kabisa na alifunikwa na tope. Nywele zake zilikuwa
ni chafu na minyoo ilikuwa ikijongea mwilini mwake .Alijaribu kuiondoakwa
mikono yake lakini kila alipo mwondoa mmoja mingine ilijizisha zaidi.Minyoo
ilikuwa na urefu karibu inchi 6-8.Neno la Bwana linasema katika Marko 9:44, "Ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki."
Ilikuwa ni ya kutisha
sana kumwona mwanamke huyu na kusikia kilio chake kwa jinsi minyoo ile kwa
hasira ilivyo kuwa inaila nyama za mama huyu. Kulikuwepo na bango la chuma
lililo kifuani mwake ambalo lisingeweza kuharibiwa na moto. Lilisomeka , "Nipo
hapa kwa ajili ya Uzinzi." Kwa jinsi ile ile ya dhambi yake,
mwanamke huyu alilazimishwa kufanya uzinzi kuzimu na nyoka wa kutisha
mnene..Nyoka huyu alikuwa na miiba mikubwa kuuzunguka mwili wake, ni kama ya
uerfu wa inchi 6-8 hivi.Nyoka humwingia mama hyu sehemu zake za siri na
kusafiri hadi mwilini mwale hadi kwenye koromeo lake. Nyoka alipo mwingilia
hivi, alianza kulia kwa makelele .
Alimwomba Bwana kwa nguvu
sana amtoe eneo lile, "Bwana, nipo hapa kwa ajili ya uzinzi, nimekuwepo
hapa kwa miaka 7, tangu UKIMWI ulipo niua. Nilikuwa na wapenzi sita6, na nipo
hapa kwa ajili ya uzinzi." Kule kuzimu alitakiwa kuirudia dhambi
yake tena na tena. Hakuna kupumzika usiku na mchana, akiteseka kwa jinsi ile
ile kila mara. Alijaribu kuunyoosha mkono wake kwa Bwana, lakini Bwana
alimwambi, "Blanca, kwako tayari
umechelewa. Minyoo itakuwa ni kitanda chako, na minyoo itakufunika." (Isaya 14:11) Wakati Bwana
alipo sema maneno hayo, blanketi la moto lilimfunika, na siku mwona tena.
Tuliendelea kutembea, tukiona
maelfu na maelfu ya watu. Walikuwepo vijan, watu wazima na wazee kabisa
wakiteseka kuzimu. Tulifika eneo lililo onekana kama eneo la bwawa la
kuogelea la moto, likiwa na maelfu ya wanaume na wanawake ndani yake. Kila
mmoja wao alikuwa na bango la chuma kifuani mwake lililosomeka: "Nipo
hapa kwa kuto toa fungu la kumi na sadaka" Nilipo soma
vile,nilimuuliza Bwana, "Inawezekanaje hili kuwa hivi, kwamba mtu yupo
hapa kwa sababu hii??" Bwana alijibu,"Ndiyo, kwasababu watu hawa walifikiri kuwa fungu la kumi
na sadaka hazikuwa ni lazima, wakati neno langu lina onyesha kuwa ni
amri." Katika Malaki 3:8-9 inasema "Je! mwanadamu atamwibia Mungu? lakini ninyi mnaniibia
mimi.Lakini ninyi mwasema .tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na
dhabihu.Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili
lote."
Bwana aliniambia kuwa
wakatim watu wake wanapo zuia fungu la kumi, inazuia kazi ya Bwana, na injili
haihubiriwi. Watu wa eneo hili wanateseka mara elfu zaidi ya wengine, kwa
sababu, walilijua neno la Bwana na hawakulitii.
Tuliendelea kutembea na
Bwana alinionyesha mtu.Niliweza kumwona kuanzia kiunoni hadi kichwani, na
nilianza kuona maono ya jinsi alivyo kufa. Jina lake ni Rogelio.
Alikuwa ndani ya gari lake wakati mtu alipo msogelea kumhubiria injili , na
kumpa Bibilia . Lakini Rogelio alikataa maonyo ya mtu yule na aliendelea kwenye
njia yake, bila ya kujua kuwa dakika chache baadaye gari lake linge pata ajali.
Liliangukia kwenye korongo, na mara alikufa.
Mara tuu baada ya ajali,
Bibilia ilifunguliwa katika Ufunuo 21:8, "Bali waoga, na wasioamini,na wachukizao, na wauaji, na
wazinzi, na wachawi, na wahao waabuo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni
katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."
Wakati Rogelio aliposoma msitari huu, alikufa na alifika kuzimu.
Alikuwepo pale mwezi
mmoja tuu na bado alikuwa na ngozi usoni mwake. Hata hivyo alikuwa akiteseka
kama wengine. Mwanzo hakujua ni kwanini alikuwepo kuzimu. Nafikiri yule mkristo
alipo mfikia pale kwenye gari yakr, ilikuwa ndiyo nafasi yake ya kipekee na ya
mwisho ya kumkubali Bwana Yesu. Kwa jinsi ile ile ambayo wengi wamepata
nafasi ya kumkubali Yesu.Leo nina kualika ufungue moyo wako kwa Yesu; Yeye tuu
ndiye njia,kweli, na uzima. (Yohana 14:6) Ni kwa yeye tuu
tunaweza kuokolewa kuingia ufalme wa Mbinguni (Matendo 4:12) Bwana alituambia pia
kuwa tuzifuate njia zake katika utakatifu na heshima. Mungu akubarik
--- (Ushuhuda wa 4) ---
Mungu awabariki kaka zangu. Wakati Bwana alipo
uchukua mkono wangu, niliweza kuona kuwa nilikuwa nimesimama kwenye mwamba, na
nyuma yetu nilimwona malaika. Tulianza kwenda chini kupitia tanuru lile kwa
mwendo wa kasi wa kutisha.Kwa haraka, niligeuka na kuona kuwa malaika alikuwa
ameondoka, na nilijisikia hofu.Nilimuuliza Bwana, "Bwana, yupo wapi
yule malaika? kwanini hayupo hapa tena?" Bwana alisema, "Hawezi kwenda pale sisi tunapo kwenda."
Tuliendelea kwenda chini
naghafla tulisimama, kama kwenye lifti. Niliona matanuru kadhaa; na tuliingia
mojawapo ambalo dada yangu Sandra ameshalizungumzia tayari. Pango ambalo
watu walikuwa wametundikwa wakining`inia na pingu mikononi mwao. Ukuta ambao
ulikuwa na watu juu yake ulikuwa ni mrefu usio na mwisho. Mamilioni ya watu walikuwa pale wakining`inia . Walikuwa
na minyoo mwili mzima. Niliangalia mbele na liona kuwa kulikuwa na ukuta
mwingine, kama ule mwingine. Nilimwambia
Bwana, "Bwana! Kuna watu wengi sana eneo hili!" Mara, andiko
liliingia akilini mwangu;ambalo silikumbuki. Bwana aliniambia, "Kuzimu na uharibifu havishibi."
(Mithali 27:20)
Tulitoka pale na mara
tulifika eneo linaloitwa, "Bonde la Masufuria ya moto(cauldrons)".
Masufuria haya yalijaa matope yanayo tokota, na tulilisogelea moja wapo. Mtu wa
kwanza ambaye nilimwona alikuwa ni mwanamke. Mwili wake ulikuwa ukipanda juu na
kushuka chini katika tope lile linalo tokota la moto, lakini Bwana alipo
mwangalia aliacha kwenda na alibaki akielea kuanzia kiunoni kwenda juu. Bwana
alimuuliza, "Mwanamke, jina lako ni
nani?" Alijibu, "Jina langu ni Rubiella."
Nywele zake zilijaa
matope yanayo tokota na nyama za mwili wake zilikuwa zina ning`inia toka mifupa
yake, ambayo ilikuwa mweusi kwa kuunguzwa. Minyoo ilimwingia kupitia mashimo ya
macho yake, ikitoka kupitia midomo yake, ikiingia tena kupitia pua zake na
kutokea masikioni. Wakati minyoo ilipo shindwa kuingia, ilifanya shimo yenyewe
kupitia eneo jingine la mwili, ambayo ilisababisha maumivu yasiyo elezeka.
Alipiga makelel, "Bwana,
tafadhali! Nitoe mahali hapa. Nirehemuu! siwezi kuendelea jinsi hii tena!
isimamishe Bwana! siwezi kuendelea tena!tafadhali nirehemu!."
Bwana alimuuliza ni kwa nini alikuwepo pale.Alisema kuwa alikuwepo pale kwa
sababu ya maringo, kitu ambacho ni saw na jinsi ilivyo kuwa imeandikwa juu ya
bango lake lililo kifuani mwake.Mkonoi mwake ni chupa ya kawaida, lakini kwake
aliiona kama ni manukato ya dhamani kubwa. Rubiella angechukua chupa ile
iliyojaa tindikali , na angejipulizia mwili wake wote. Hii ilimsababishia nyama
yote iliyo puliziwa kuyeyuka kumsababishia maumivu makubwa sana.
Alipiga kelele kwa Bwana,
"Bwana tafadhali, nirehemu! siwezi kuwepo tena hapa ! kwa sekunde moja
tuu Bwana." Sisemi kuwa ni
dhambi kutumia manukato, lakini Bwana alituambia kuwa mwanamke yule alikuwepo
pale kwa ajili ya maukato yake, kama vile neno la Mungu linavyo tuambia katikaI
am not saying that it is a sin to use a perfume, but the Lord told us that the
woman was there because of her perfume, as the Word of the Lord tells us in Kumbukumbu
la Torati 5:7 " Usiwe na miungu mingine
ila mimi." Alikuwepo pale kwasababu ya uzuri wake, manukato, na
maringo yalikuwa ndicho kitu cha kwanza katika maisha yake. Hata hivyo,
Bwana Yesu ni mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana! Anatakiwa kuwa wa kwanza
katika maisha yako; hii ndiyo maana alikuwepo pale. Kwa huzuni, Bwana
alimwangalia na kusema , "Rubiella,
unechelewa, minyoo itakuwa kitanda chako, na minyoo itakufunika."
Wakati Bwana aliposema hivyo, blanketi la moto lilimfunika kabisa. Wakati wmili
wake ukiwa umefunikwa kabisa ndani ya sufuria lile la moto, alikuwa akitesema sana.
Tulitoka pale na kwenda mbali zaidi eneo lenye milango
imkubwa .Tulipokuwa tumeifikia, ilitufungukia yenyewe. Upande mwingine tuliona
pango kubwa. Nilipo angalia juu niliona rangi tofauti za mwanga
zikitembea kama mawingu ya moshi.Ghafla
tulisikia mziki wac; salsa, ballenato, rocki, na aina tofauti ya miziki
mashuhuri ambayo watu huisikiliza kwenye redio. Bwana aliuelekeza mkono wake na
tuliona, mamilioni na mamilioni ya watu wakiwa wametundikwa na minyororo
mikononi mwao. Walikuwa wakiruka ruka kama
wanyama ndani ya moto.
Bwana alituangalia na alisema: "Angalia huu ni mshahara wa wacheza mziki."
Watakuwa wakiruka kama wanyama juu na chini
sawa na mapigo ya miziki. Kama ni
salsa inapigwa, walitakiwa kuruka kwa mapigo yale, kama
aina nyingine ya mziki ikipigwa, walitakiwa kuruka sawa na mapigo yake.Hawawezi
kamwe kuacha kuruka.Lakini mbaya zaidi, viatu vyao vina misumazi ya inchi6
chini yake. Wakati wanaporuka inawangia miguuni mwao na hawatakuwa na nafasi ya
kupumzika.Wakati mtu anapotaka kuacha, pepo lingekuja maramoja na kumchoma na
mkuki, likiwalaani na kusema, "Msifuni yeye
sasa! Huu ndio ufalme wenu sasa, msifuni Shetani! msifuni! huwezi kuacha,
msifuni!ni lazima umsifu !lazima uruke! lazima ucheze!Uwezi kuacha hata kwa
sekunde moja."
Ilikuwa hatari kuwa wengi wa watu wale walikuwa ni
wakristo waliomjua Bwana,lakini walikuwa kwenye madisko ya usiku walipo kufa.
Labda unauliza, "Wapi Bibilia inasema kwamba ni vibaya kucheza?"
Katika Yakobo 4:4, Neno la Bwana linasema:: "
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui na Mungu? basi
kila atakaye kuwa rafiki wa dunia kuwa adui wa Mungu."
Pia katika 1
Yohana 2:15-17, "Msiipende dunia, wala
mambo yaliyopo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani
yake, maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho,
na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.Na dunia
ianpita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata
milele." Kumbuka dunia itapita, vitu vyote hivi vitaharibika,
lakini yule atendaye mapenzi ya Mungu atadumu milele.
Rafiki zangu na kaka
zangu, tulipo acha eneo hili, tuliona kitu kama daraja lililo igawanya kuzimu
katika maeneo tofauti ya mateso.Tuliiona roho ikipita kwa miguu juu ya daraja.
Ilionekana sawa na mdoli tuliyo iona duniani; tunaiita mikokoteni ya dhamani.
Ina nywele za rangi za aina mbali mbali, zina nyuso za mzee lakini mwili wa
mtoto, bila maeneo ya siri. Macho yaliyo jaa uovu. Bwana alituelezea kuwa hizi
ni roho za upotovu. Roho hii ilikuwa na mkuki mikononi na ilikuwa ikitembea kwa
maringo katika daraja lile kama vile ni mwana wa mfalme.
Alipo kuwa anatembea,
aliwachoma watu chini kwa ule mkuki wake. Alikuwa akiwalaani akisema,"Mnakumbuka siku zile mlipo kuwa nje ya makanisa ya
kikristo na mlikataa kuingia ndani? Mnakumbuka siku zile walipo wahubiria na
hamkutaka kusikiliza? Mnakumbuka wakati walipo wagawia vipeperushi vya
injili na mkavitupa mbali?" Roho hizi zilizo potea
hujitahidi kufunika maeneo yakle ambayo masikio hukaa. Huwajibu mapepo yale,
"Nyamaza! Nyamaza! usiniambie tena! sitaki kujua
zaidi, nyamaza!" Hata hivyo, mapepo yale hupenda kufanya vile
kwakuwa huwaingizia maumivu watu wale kwenye nafsi zao.
Tuliendelea kutembea na Bwana.
Kwa kule kuangalia umati wa watu, tuligundua kuwa mtu mmoja alikuwa akipiga
makelele zaidi ya wengine waliokuwa wakiungua pale.Alikuwa akisema, "Baba,
Baba, nirehemu!" Bwana alikuwa asisimane lakini aliposikia neno
"Baba" Alisisimka na kugeuka. Yesu alimwangalia na
kumuuliza,"Baba? Unaniita Baba?
Hapana, mimi siyo Baba yako na wewe kamwe sio mtoto wangu. Kama ungekuwa mtoto
wangu, ungekuwa sasa na mimi katika Ufalme wa Mbinguni.Ninyi ni wana wa
Shetani baba yenu." Ghafla blanketi la moto lilikuja
na kabisa lilimfunika mwili wake.
Bwana alituelezea habari
ya maisha ya mtu yule. Mtu yule alimwita Baba kwa sababu aliwahi kumjua .
Alikuwa akienda kanisani na alikuwa akilisikiliza neno la Mungu, na alikuwa
amepokea ahadi nyingi za Mungu. Hivyo tuliuliza, "Nini basi kilitokea
Bwana? Kwanini basi yupo hapa leo?" Bwana alitujibu,
"Alikuwa akiishi maisha ya aina mbili;
moja nyumbani moja kanisani. Alifikiria moyoni mwake, 'Hapana mtu anaye ishi
karibu yangu, sii mchungaji, wala ndugu yeyote, hivyo naweza kufanya chochote
ninacho taka. Lakini alisahau kuwa jicho la Bwana lipo juu ya njia zetu zote
kwamba hakuna mtu anaye weza kumdanganya au kujificha mbele za Bwana."
Neno la Bwana linatuambia
kuwa, "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi;
Kwakuwa chochcote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna."
(Wagalatia 6:7) Mtu huyu alikuwa
akiteseka mara alfu zaidi ya wengine. Alikuwa akilipwa hukumu mara mbili: moja
kwa ajili ya dhambi zake na nyingine ni kule kufikiri kuwa anaweza kumdanganmya
Bwana.
Leo, watu wana jaribu
kupima ukubwa wa dhambi; wanafikiri kuwa kulawitiana, kuua ni dhambi
kubwa zaidi ya kusema uongo au kusengenya. Lakini mbele ya macho ya Bwana,
dhambi zote hizi zina uzito mmoja na malipo sawa. Bibilia inatuiambia kuwa,
"Mshahara wa dhambi ni mauti" "na
roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa." (Warumi 6:23) (Ezekieli 18:20) Rafiki zangu na
kaka zangu, nina waalika sasa kuukubali mwaliko wa Yesu. Yesu ameunyoosha mkono
wake wa rehema kwako kama ukitubu.Neno la Bwana linatuambia kwamba yule atakaye
geuza njia zake na kutubu atapokea rehema.Ni vizuri zaidi ukaamini sasa, kuliko
kusubiri na kukuta njia ngumu mbeleni. Mungu
akubariki.
--- (Ushuhuda wa 5) ---
Neno la Mungu linasema katika Warumi
6:23 " Kwa maaana mshahara wa dhambi ni
mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Tulipo kwenda chini
mahali pale, nilisikia maumivu na uzoefu wa kifo. Nilikuwa nimeogopeshwa sana
na kile nilicho kiona.Niligundua kuwa kuliwa na watu wengi, wengi sana ; wote
walikuwa wakilia na kupiga makelele.Lilikuwa ni giza tupu, , lakini katika
uwepo wa Bwana,giza lilitoweka.Tuliona maelfu na maelfu ya roho zote
zikilia kuomba msaada na rehema.Walikuwa wakilia kwa Bwana kuwaondoa eneo
lile. Tulijisikia pia maumivu kwa sababu tulijua Bwana alikuwa akiteseka
sana kila alipo waona.
Wengi walilia
kwa Bwana kuwaondoa mahali pale angalau kwa sekunde
moja tuu. Bwana angewauliza, "Kwa nini
unataka kutoka nje ya hapa?", na wangelijibu, "Kwa
sababu ninataka kuokoka! Nataka kutubu na kuokoka!" Hata
hivyo ilikuwa kwao tayari wamechelewa.
Wapendwa watu
mnaonisikiliza sasa, sasa ndio nafasi pekee ya sisi kuchagua eneo letu la
umilele. Unaweza tuu kuchagua umilele wa wokovu au wa hukumu.
Tulikwenda chini kwa
zaidi. Niliona kuwa sakafu tuliyokuwa tunatembea juu yake, ilikuwa
imeharibiwa na moto; na tope na moto lilikuwa linatoka ndani yake. Kulikuwepo
pia na harufu ya kutisha kila mahali. Tulijisikia vibaya sana na mahangaiko
kutokana na harufu na makelele ya watu wote.
Tulimwona mtu, kwa mbali
ambaye alikuwa amezama chini kwenye tope la moto.Alipo toa mkono wake. nyama
toka toka mifupa yake zilidondoka chini kwenye tope.Tuliweza kuona mvuke wa
kikahawia ndani ya mifupa yake, hivyo tulimuuliza Bwana ninini kile. Aina
hii ya mvule upo ndani ya kila mtu kuzimu.Bwana alituambia ni nafsi zao zilizokamatwa
ndani ya miili yenye dhambi; Kama ilivyo andikwa katika Ufunuo 14:11 "Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na
milele, wala hawana raha mchana wala usiku, nao wamsujudia huyo mnyama na
sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake."
Tulianza kuelewa vitu
vingi ambavyo tulividharau duniani;Jambo la muhimu, ujumbe wa karibu zaidi ni
kuwa, maisha yetu duniani yana amua ni wapi tutakapo tumikia umilele wetu baada
ya kufa.
Tulipo kuwa tunatembea
tukiwa tumeshikana mkono na Bwana, tuligundua kuwa kuzimu ina sehemu nyingi
sana yenye mateso mbalimbali. Tulifika eneo lenye vyumba vingi na roho nyingi
zinateseka huko. Roho hizi zilikuwa zinateswa na mapepo mengi ya aina nyingi.
Mapepo yangeweza kuzilaani zile roho, kwa kusema, "Ninyi masikini mlio laaniwa, msifuni Shetani!
Mtumikieni kama vile mlivyo fanya mlipo kuwa duniani.!"
Roho zile ziliteseka sana kutokana na minyoo ile; na moto ulikuwa ni kama
tindikali juu ya mwili wote.
Tuliwaona watu wawili
ndani ya chumba kile cha jela, kila mmoja alikuwa ameshika kisu na anamsumbua
mwenzake. Wangelisema, "Wewe masikini mlaaniwa! ni kwasababu yako ndiyo
maana nipo hapa! Ulinifanya nije hapa kwasababu ulinipofusha nisujue ukweli na
hukuniruhusu kumjua Bwana! Hukuniruhusu kumpokea! Mara nyingi nilipata nafasi
lakini hukuniruhusu kumkubali! Ndiyo sababu nipo hapa leo, nateswa usiki na
mchana!"
Kupitia maono, Bwana
alituonyesha maisha yao duniani, Tuliwaona wakiwa baa ya pombe pamoja.
Mazungumzo yalianza yaliyo pelekea kupigana. Walikuwa tayari walevi. Mmoja
alichukua chupa iliyo vunjika na mwingine alitoa kisu. Walipigana mpaka wote
wakawa wamejeruhiwa sana na wakafa.Watu hawa wawili waliwekewa kulirudia tukio
hili milele.Waliteseka pia na kumbu kumbu zao kuwa walikuwa ni marafiki sana
duniani, kama mtu na nduguye wakipendana.
Nataka kukuambia leo
kuwa, kuna rafiki mmoja tuu wa kweli, na jiana lake ni Yesu wa Nazarethi
. Yeye ni rafiki wa kweli. Ni rafiki mwaminifu, aliye pamoja nawewe katika muda
wote.
Tulipo endelea kutembea
tulimwona mwanamke ndani ya chumba kingine, alikuwa akinivingirisha kwenye lile
tope. Nywele zake zilikuwa chafu na zenye tope. Ndani ya chumba kile
alikuwepo nyoka mnene mkubwa.Alikuwa anamsogelea na kumzunguka mwili wake, na
alianza kumwingilia mwilini mwake akianzia sehemu zake za siri. Alilazimishwa
kufanya uzinzi na yule nyoka. Kwenye eneo hili, wanaume na wanawake
waliokuwa wazinzi walilazimishwa kufanya uzinzi . Hata hivyo walilazimika
kufanya hivyo na majoka yale yaliyofunikwa na vitu vikali mwili mzima kama
chuma kikali cha inchi 6. Nyoka aliuharibu kabisa mwili wa mwanamke yule
kila mara alipo mwingilia. Alilia sana kwa Bwana na kumwomba kusimamisha hali
ile.Hakutaka kuteseka tena. "Simamisha! Sitaki kufanya
tena!tafadhali simamisha hii hal!" Alimwomba Bwana amhurumie kila
wakati nyoka alipo mwingilia na muuharibu mwili wake tena na tena.
Tulijitahidi kuyafunga
masikio yetu tusisikie kilio chake, lakini bado tulimsikia.Tulijaribu kwa nguvu
zaidi kufunga masikio yetu , lakini haikusaidia. Tulisema Bwana, "Tafadhali
Bwana, hatutaki kuona na kusikia hivi tena! tafadhali!" Bwana alitujibu,
"Ni muhimu muone haya, ili muwaeleze
wengine. kwa sababu watu wangu wanaangamizwa, watu wangu wanaukataa wokovu
halisi, njia ya kweli ya wokovu."
Tuliendelea kutembea na
tuliona ziwa kubwa lenye watu maelfu na maelfu ndani yake katikati ya mioto.Walitupungia
wakiomba msaada, lakini kulikuwa na mapepo mengi yakiruka juu ya eneo
lile.Mapepo haya yalikuwa yanatumia mikuki yenye vichwa kama
S- kuwaumiza watu wale waliokuwa wakiunguzwa katika lile ziwa.
Mapepo yaliwatania na kuwalaani yakisema, "Ninyi
masikini mlio laaniwa! Sasa ni lazima kumwabudu Shetani! Msifuni, msifuni kama
mlivyo fanya wakati mlipo kuwa duniani!" Kulikuwepo watu
maelfu kwa maelfu. Tuliogopa sana,tulihisi kama tusingeushika mkono wa Bwana
tungebaki katika eneo lile la kutisha. Tuliogopeshwa na vitu tulivyo kuwa
tunavihisi.
Kwa mbali tulimwona mtu
aliyesimama, akiwa kwenye maumivu makubwa na huzuni. Alikuwa na mapepo mawili
yakiruka juu yake yakimtesa. Yangeweza kuchimbia mikuki yao mwilini mwake na
kutoa mbavu zake. Yalikuwa pia yakimtania kila mara. Zaidi ya yote Bwana
alinionyesha kuwa alikuwa akiteseka kwa hofu ya kila siku juu ya familia yake
aliyo iacha duniani. Mtu huyu hakutaka familia yake ije mahali pale pa
mateso. Aliogopa kwa sababu hakuwahi kuwapa ujumbe wa wokovu. Aliteseka
zaidi kwa kukumbuka kuwa wakati fulani walikuwa na nafas.Alikuwa mtu muhimu
katika ile familia ambaye angeweza kuwapa ujumbe ule, lakini aliamua
kuudharau ujumbe ule na sasa alikuwa akihofia juu ya watoto wake na mke
wake.
Mateso yaliendelea pale
ambapo mapepo yalipo mkata mikono yake, aliangukia kwenye matope ya moto.
Kwasababu ya maumivu toka tope lile la moto, alijongea kama vile minyoo toka
eneo moja hadi jingine. Nyama zilimtoka mwilini mwake sababu ya ule moto.
Alianza baadaye kutambaa kama nyoka ili atoke pale. Lakini kila mara
alipojaribu kwenda, mapepo yalimsukuma na kumrudisha pale na alizama zaidi
kwenye lile tope.
Baadaye tuliona idadi ya
mapepo eneo moja.Kitu fulani kilinivuta kuangalia, niliona kuwa mojawapo ya
mapepo lilikuwa halina bawa lake moja. Nilimuuliza Bwana, "Bwana,
kwanini pepo hili halina bawa moja?" Bwana alisema, "Pepo lile lilitumwa duniani kwa lengo moja, lakini
halikukamilisha kazi yake, na lilikemewa na mmoja wapo wa watumishi wa Mungu na
kurudishwa kuzimu. Baadaye Shetani alikuja na kuliadhibu, na kulikata moja ya
mabawa yake." Ndipo tulipo gundua kuwa kama wakristo,
tuna mamlaka ya kukemea mapepo yote na mamlaka zote.
Mpendwa rafiki unaye
sikiliza maneno haya sasa hivi, ushuhuda huu sii kwa ajili ya kukuhukumu bali
kwa wokovu; hivyo unaweza kujipima mwenyewe na kuona hali ya roho yako mbele za
Bwana. Hii ndivyo ilivyo ili uweze kubadili njia zako kwa wokovu na sio kwa
hukumu. Sasa hivi inua moyo wako kwa Bwana na utubu dhambi zako, ili kama
Bwana akija sasa hivi uweze kwenda naye badala ya kwenda eneo lile la mateso
mahali penye kilio na kusaga meno. Hapa utajua ni kwanini Yesu alilipa gharama
kubwa vile pale msalabani Kalvari.
Tuliona watu wengi kuzimu
ambao hawakujua ni kwa nini walikuwepo pale. Maisha yao yalijaa mambo ambayo
hawakuwahi kujua kuwa ni dhambi. Mpendwa rafiki yangu, jipime mwenyewe!
usifikiri kuwa kudanganya, kuiba, maringo ni vitu sahihi vya kufanya! vyote
hivi ni dhambi mbe;le za macho ya Bwana! Mpendwa
kaka, jeuka na acha kufanya vitu hivi!Ninakupa ujumbe huu ili uache kufanya
dhambi kwa kudhamiria, na kuuangalia zaidi uso wa Bwana.
--- (Ushuhuda wa 6) ---
Zaburi
62:12 "Na fadhili ziko kwako, Ee
Bwana; maana ndiwe umlipaye kila mtu sawasawa na haki yake."
Asubuhi Bwana alitutembelea pale chumbani,
alitushika mkono na tulianza kwenda chini.Roho yangu ilikuwa imejawa na hofu,
siwezi hata kuielezea.Nilifahamu tuu kuwa siwezi kuuachia mkono wa mwokozi
wangu.Nilijisikia kuwa Yesu ni maisha yangu , mwanga wangu na kila tumaini
langu lilikuwa kwake; kama sivyo ningebakia mle kuzimu.Sikuwahi kuwaza
kama ningewahi kwenda eneo lile.Sikuamini pia kama eneo kama hili lipo.Japo ni
Mkristo nilifikiria kuwa kuna eneo linaloitwa Pagatori na labda ndilo kuzimu,
lakini Mungu alinionyesha ukweli wa Kuzimu.
Tulipofika kuzimu,nilijisikia mshituko wa eneo lile.Na
mapepo yote pale yalikimbia kujificha, kwasababu hakuna hata mojawapo ya pepo
linalo weza kusimama mbele ya uwepo wa Yesu..Tulisikia roho zilizo kamatwa
kuzimu zikipiga makelele ya nguvu, kwasababu walijua kuwa Yesu wa Nazarethi
yupo pale. Walijua wote kuwa yupo mtu mmoja tuu anaye weza kuwatoa eneo lile.
Walikuwa na matumaini hayo, japo ni matumaini ya uongo.
Tulitembea tukiwa tumeshikana mikono na Yesu, na
tulifika eneo la uzinzi. Yesu aligeuka kumwangalia mwanamke ambaye alikuwa
amefunikwa kabisa na moto. Wakati Yesu alipo mwona, alianza kutoka mle motoni
taratibu, japo maumivu yake hayakusimama.Tuliweza kuona kuwa alikuwa yuu uchi
kabisa na kuweza kuona mwili wake mzima. Mwili wake ulikuwa mchafu sana, na alikuwa
ananuka.. Nywele zake zilikuwa zimevurugika sana na alikuwa na tope la rangi ya njano na
kijani juu yake.Hakuwa na macho na midomo yake ilikuwa imechanika. Hakuwa na
masikio, ni machimo tuu. Kwa mikono yake, iliyo mifupa iliyo geuka kuwa
mweusi kwa moto, aliichukua ile nyama iliyo kuwa inadondoka toka usoni mwake,
na kujaribu kuirudishia. Lakini jambo hili lilimpa maumivu mabaya zaidi.
Alitetemeka na kulia zaidi; kilio chake
hakikukoma.Alikuwa amejaa minyoo, na alikuwepo joka kubwa lililo jivingirisha
mkononi mwake. Lilikuwa ni nene sana
na lenye miiba mwili mzima.Mwanamke huyu alikuwa na alama ya namba 666 iliyo
chimbiwa mwilini mwake; namba
ya mnyama iliyo tajwa katika kitabu cha Ufunuo. (Ufunuo
4:9-11) Alikuwa pia amevaa bango la chuma kifuani mwake, iliyo
tengenezwa na madini yasiyo fahamika, haikuwa inaweza kuteketezwa na moto.. Juu
ya bango lile iliandikwa jambo fulani kwa lugha ngeni, lakini tuliweza
kuielewa.Ilisomeka, "Nipo hapa kwa ajili ya uzinzi."
Yesu alipo mwona
alimuuliza, "Elena, kwanini upo eneo
hili?" Wakati akijibu, Elena alikuwa akijipinda
kutokana na maumivu yake. Alisema kuwa yupo pale kutokana na uzinzi.Alimwomba
Bwana msamaha tena na tena
Baadaye tulianza kuona
tukio la kifo chake.Alipo kufa alikuwa akifanya mapenzi na mmoja wa wapenzi
wake, kwa sababu alifikiri kuwa mwanamke aliye kuwa anaishi naye alikuwa
amesafiri.Hata hivyo mwanaume yule alirudi toka kazini na alimkuta akiwa
kitandani pamoja na mwanaume mwingine,Mwanaume yule alikwenda jikoni na
kuchukua kisu kikubwa na alimpiga nacho Elena nyuma mgongoni mwake.Elena
alikufa na alichukuliwa kuzimu, vilevile kama alivyo kufa; bado yupo uchi
kabisa.
Kule kuzimu kila kitu
kinaendelea, na bado anacho kile kisu mgongoni mwake, kikimsababishia maumivu
makubwa.Wakati huu alikuwa tayari yupo kuzimu kwa miaka 7 na aliweza kukumbuka
kila tukio la maisha yake na kifo chake.Aliweza hata kukumbuka wakati mtu
fulani alipo mhubiria habari za Yesu; kwamba ndiye pekee anaye weza kumwokoa.
Lakini sasa ilikuwa tayari amechelewa sana na kwa kila aliyepo kuzimu.
Neno la Bwana
linazungumza sana juu ya uzinzi, na lipo wazi sana. Uzinzi ni kuwa na uhusiano
wa kimapenzi nje ya ndoa. 1
Wakorintho 6:13 "Vyakula ni kwa tumbo,
na tumbo ni kwa vyakula;lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula.
Lakini mwili sii kwa zinaa, bali ni kwa Bwana naye Bwana ni kwa mwili."
pia katika 1
Wakorintho 6:18 "FIkimbieni zinaa. Kila
dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake mwewnyewe, lakini yeye afanyaye
zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."
Wakati Yesu alipo maliza
kuzungumza naye, alifunikwa na blanketi kubwa la moto na hatukumwona tena.
Lakini tulisika sauti ya mwili wake ukiungua na makelele yale ya kutisha,
siwezi hata kuyaelezea vizuri kwa maneno.
Kwa jinsi tulivyo kuwa
tunaendelea kutembea na Bwana, alituonyesha watu wote pale: waabudu sanamu, wale
wanao tumia na kufanya uchawi,wasio safi,washerati, waongo, na wafiraji.
Tuliogopa sana, kitu pekee tulicho taka kufanya ni kuondoka pale.Lakini Yesu
aliendelea kusema kuwa ni muhimu kuendelea kuangalia ili tuwaeleze wengine, ili
waweze kuamini.
Tuliendelea na Yesu na
tulimshika mkono wake kwa nguvu zaidi.Tlifika eneo ambalo
lilinishangaza.Tulimwona kijana mdogo , wa miaka 23, akiwa ameinuliwa juu
katikati ya moto. Hatukuweza kuona vizuri mateso yake ni yapi, lakini ile namba
666 ilikuwa imechimbiwa mwilini mwake. Alikuwa pia na bango lile kifuani mwake
lililosomeka,"Nipo hapa kwa kuwa wa kawaida." Alipo
mwona Yesu, aliunyoosha mkono wake kwa Yesu akiomba rehema. Neno la Mungu
linasema katika Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo
kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti."
Tuliposoma lile bango
lililo sema, "Nipo hapa kwa kuwa wa kawaida", Tulimuuliza
Bwana"Bwana, inawezekanaje!? Inawezekana mtu akaja eneo hili kwa
sababu hii?" Ndipo Yesu akamuuliza, "Andrea,kwa nini upo eneo hili?"
Alijibu, "Yesu, nilipo kuwepo duniani, nilifikiri kuwa , kuua, kuiba
zilikuwa ndizo dhambi tuu, na ndiyo sababu sikuwahi kujaribu kuja karibu yako."
Katika Zaburi 9:17 inasema "Wadhalimu watarejea kuzimu, naam mataifa yote wanao
msahau Mungu."
Andrea alifanya kosa kubwa kwa kugawa dhambi, kama
wengi wa watu wanavyo fanya leo.Bibilia ipo wazi sana inaposema mshahara wa
dhambi ni mauti , lakini karama ya Mungu ni uzima wa milele.(Warumi
6:23) Zaidi, wakati Bibilia inapo zungumza habari za dhambi, haigawi
dhambi, kwa sababu zote ni dhambi tuu. Andrea alikuwa na nafasi ya kumjua na
kumpokea Yesu, lakini hakuichukua nafasi ile ambayo Mungu alikuwa amempa.
Labda alikuwa na nafasi elfu kumjua Bwana, lakini hakutaka kumjua na hii ndiyo
sababu alikuwa pale. Baadaye blanketi kubwa la moto lilimfunika na hatukumwona tena.
Tuliendelea kutembea na
Yesu. Kwa mbali tuliona kitu fulani kikidondoka kama maumbo fulani
hivi.Tulipo sogea karibu, tuliona kuwa ni watu wapya waliokuwa wakiingia kuzimu
muda ule.Watu ambao ndio tuu wakekufa duniani kabla hawajampokea Yesu miyoyoni
mwao, walikuwa wakiingia kuzimu.
Tulimwona kijana mmoja,
mapepo mengi yalimkimbilia na kuanza kuuharibu mwili wake. Mara mwili wake
ulianza kujawa na minyoo. Alipiga kelele, "Hapana! Ni nini
hii? Acha! Sitaki kuwa eneo hili! Simamisha hii! Hii lazima
itakuwa ni ndoto!" Hakujua kuwa amekufa, na ya kuwa amekufa bila
ya Yesu moyoni mwake.Mapepo yalikuwa yakimchezea na kuuharibu mwili wake.
Baadaye namba 666 ilitokea kwenye upaji wa uso wake, na bango la chuma kifuani
mwake.Japo hatu kuweza kuona sababu ya yeye kuja kuzimu lakini tulijua kuwa
hataweza tena kutoka mle.
Bwana alituambia kuwa ,
mateso ya wote walio kuzimu yatakuwa makubwa zaidi siku ya hukumu.Kama
wanateseka kwa jinsi ile ya kutisha na ya kuogopesha sasa, siwezi kufikiria
jinsi gani watateseka siku ile ya hukumu.
Hatukumwona mtoto yeyote
pale.Tuli waona vijana maelfu kwa maelfu; wanaume kwa wanawake wa mataifa
mengi. Hata hivyo kuzimu hakuna utaifa au tabaka, wote wanakuja hapa kuteswa na
kuhadhibiwa. Kuna kitu kimoja ambacho kila mtu pale alikihitaji, na hicho
ni nafasi tuu ya kutoka mle ndani, angalau kwa sekunde. Wanataka pia
kupata angalau tone la maji kuuburudisha ndimi zao., kama vile habari ile ya
tajiri kwenye Bibilia. (Luka 16:19) Lakini hii hili
haliwezekani tena kwao, walikwisha chagua ni wapi watakapo kaa milele.
Walichagua umilele bila ya Mungu.Mungu kamwe hampeleki mtu yeyote kuzimu, kila
mmoja huenda kuzimu kutokana na matendo yake mwenyewe katika Wagalatia 6:7 "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho
chote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna."
Leo una nafasi kubwa ya
kubadilisha mahali pako pa umilele.Yesu bado anapatikana sasa, na Bibilia
inasema kuwa wakati tukiwa hai bado tuna matumaini.Leo una uhai, usikose nafasi
hii, inaweza ikawa ni ya mwisho kwako.
Mungu akubariki.
Kwa shuhuda zaidi tembelea ukurasa wa ushuhuda....
No comments:
Post a Comment