Nov 23, 2014

Ufunuo wa Yesu Kuhusu Kuzimu na Mary K Baxter



Karibu  ndugu msomaji na mfuatiliaji wa shuhuda mbalimbali...ufuatao ni ushuhuda wa dada Mark K Baxter, ushuhuda huu mara ya kwanza ulikujia kwa lugha ya kingereza na sasa unakujia tena kwa lugha ya kiswahili...nnakusihi unapousoma upate nafasi katika roho yako.....Mungu wa mbinguni akubariki...

Sikiliza ushuhuda wa moja kwa moja juu ya
uwepo Halisi wa Kuzimu. Mary Katherine
Baxter alichaguliwa na Mungu ili kuujulisha
ulimwengu juu wa UHALISI wa Kuzimu. Yesu
Kristo alimtokea Mary Baxter wakati wa usiku
siku 40 mfululizo na kumtembeza kuzimu na
Mbinguni. Alitembea, na Yesu, na kuona
mambo ya kutisha ya Kuzimu na alizungumza
na watu wengi.Yesu alimwonyesha ni kitu gani
kinatokea roho zinapokufa na mambo gani
yanatokea kwa wasioamini na watumishi  wa 
Mungu ambao hawatii wito walioitiwa.


Neno la Awali

Marcus Bach alisema kwamba mara nyingi vitabu ni kama watoto wa akili, wala hakukosea. Sio
kama watoto wa nyama na damu, watoto hawa, wanaozaliwa kwa kupanga au kwa bahati
wamepangiwa maisha yao wenyewe. Kuishi kwao katika ulimwengu huu kunafanana na watoto
wengine. Hisia zote za kibinadamu ni zao. Si ajabu hofu yao ya siri ni kwamba siku moja watawekwa
kando na kusaulika moja kwa moja.
Tofauti na vitabu vingine, ninaamini kwamba Roho Mtakatifu amefanya maandishi haya kuwepo kwa
muda na milele. Ushuhuda na ujumbe huu ni wa muhimu sana kwa mwili wa Kristo. Ninaamini
kwamba upako wa Mungu utakuwa juu ya kitabu hiki na kumhudumia kila mtu asomaye yaliyomo.

Wakfu

Kazi hii imewekwa wakfu kwa utukufu wa Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu,
bila Yeye kitabu hiki kisingewezekana kuwepo.
 
Utangulizi

Ninatambua kwamba bila nguvu za Bwana Yesu Kristo, kitabu hiki au kingine
kinachoshughulikia na maisha baada ya kifo kisingeandikwa.Yesu peke yake ndiye aliye
na funguo za Kuzimu na amelipa gharama za kutuingiza mbinguni.

Niligundua  kwamba  kuandika  kitabu  hiki  ilikuwa  ni  kazi  ndefu,  ya    upweke,  na  ngumu.
Kwa  kweli  kitabu  hiki  kimesubiri  miaka  mingi  kufunuliwa.  Ufunuo  kutoka  kwa  Bwana
ulinijia  mwaka  1976.  Ilinichukua  miezi  minane  kuuandika  katika  karatasi.  Uandikaji  wa
rasimu  ulichukua  miaka  mingi  na  uwekaji  wa  vifungu  vya  Maandiko  hatua  kwa  hatua
ilinichukua  mwaka  mwingine  zaidi.  Kukamilisha  kitabu  kulichukua  msimu  wa  baridi  wa
1982  na  mwaka  1983.  Vile  vile  kwa  muda  wa  siku  thelathini,  Yesu  alinichukua  hadi
Kuzimu wakati wa usiku, zikafuata siku kumi za kutembelea mbinguni wakati wa usiku.
Sasa  naona  kwamba  Bwana  alikuwa  ananiandaa  kuandika  kitabu  hiki  tangu  nilipokuwa
mtoto  mdogo  nilipokuwa  naota  mambo  ya  Mungu.  Baada  ya  kuzaliwa  mara  ya  pili,
nilikuwa na mapenzi sana kwa waliopotea na nilikuwa natamani kuona roho zikiokolewa.
Baadaye  Bwana  alinitokea  mwaka  1976  na  kuniambia  kwamba  nilikuwa  nimechaguliwa
kwa ajili ya kazi maalum, Aliniambia,
Mwanangu,  nitajithibitisha  kwako  na  kuwatoa  watu  kutoka  gizani  na  kuwaleta  nuruni.
Kwa  maana Bwana Mungu amekuchagua kwa kusudi, kuandika na  kuweka  kumbukumbu
ya mambo nitakayokuonyesha na kukuambia.
"Nitakufunulia  uhalisi  wa  kuzimu,  ili  wengi  waokolewe,  wengi  watatubu  njia  zao  mbaya
kabla hawajachelewa."
Roho  yako  itachukuliwa  kutoka  kwenye  mwili  wako,  na  mimi,  Bwana  Yesu  Kristo,  na
kupelekwa  kuzimu  na  sehemu  nyingine  nitakazopenda  kukuonyesha.  Vile  vile
nitakuonyesha maono ya mbinguni na mahali pengine na kukupa mafunuo mengi.


Kwa  kusudi  hili  ulizaliwa,  kuandika  na  kueleza  mambo  niliyokuonyesha  na  kukuambia.
Maana mambo haya ni uaminifu na kweli. Wito wako ni kuufanya ulimwengu ujue kwamba
kuna  kuzimu,  na  kwamba  Mimi,  Yesu,  nilitumwa  na  Baba  ili  kuwaokoa  kwenye  mateso
haya.

                                                             Sura ya  1
Kwenda Kuzimu
Mwezi Machi 1976 nilipokuwa naomba nyumbani, nilitembelewa na Bwana Yesu. Nilikuwa
nikiomba  katika  Roho  kwa  siku  kadhaa  ambapo  mara  nilihisi  uwepo  halisi  wa  Mungu.
Nguvu yake na utukufu wake uliijaza nyumba. Mwanga mkali ulikijaza chumba nilimokuwa
naomba, na hali ya kujisikia vizuri ilinijia.
Mwanga  ulikuja  kama  mvuke,  ukiviringika  na  kujikunja  na  kujikunjurua  tena.  Lilikuwa
jambo la ajabu. Ndipo sauti ya Bwana ikaanza kuzungumza nami.
Alisema,  "
Mimi  ni  Yesu  Kristo,  Bwana  wako,  nataka  kukupa  ufunuo  wa  kuwaandaa
watakatifu  kwa  ajili  ya  kurudi  kwangu  na  kuwageuza  wengi  kuelekea  kwenye  haki.
Nguvu za giza ni halisi na hukumu zangu ni halisi.
"Mwanangu,  nitakupeleka  kuzimu  kwa  Roho  Yangu,  na  nitakuonyesha  mambo
mengi  ambayo  nataka  ulimwengu  uyajue.  Nitaonekana  kwako  mara  nyingi;
nitaichukua roho yako nje ya mwili wako na nitakupeleka kuzimu kihalisi.
"Nataka uandike kitabu na ueleze maono yote na mambo yote nitakayofunulia. Mimi
na  wewe  tutatembea  kuzimu  pamoja.  Andika  mambo  haya  yaliyopo  na
yatakayokuja.  Maneno  yangu  ni  hakika,    kweli,  aminifu.  Mimi  Ndimi,  wala  hakuna mwengine badala yangu"
"Bwana wangu
” nililia, “
Unataka nifanye nini
?” Kila kitu ndani yangu kilitaka kumlilia Yesu,
kukiri uwepo  wake.  Nikijitahidi  sana  kueleza niseme kwamba upendo ulinifunika.  Ulikuwa
ni  upendo  mzuri,  wa  amani,  wa  furaha,  wenye  nguvu,  kuliko  nilivyowahi  kuhisi  wakati
wowote.
Sifa  za  Mungu  zilianza  kunimiminika.  Pale  pale  nilitamani  kumpa  maisha  yangu  yote
ayatumie,  kusaidia  kuwakoa  watu  katika  dhambi.  Nilijua,  kwa  Roho  wake,  kwamba
alikuwa  Yesu  Mwana  wa  Mungu  aliyekuwa  chumbani  pamoja  nami.  Sipati  maneno  ya
kuelezea uwepo wake. Lakini najua kwamba najua kwamba alikuwa ni Bwana.

"angalia , mwanangu"
Yesu alisema
,
Ninakuchukua kwa roho wangu hadi kuzimu ili
uweze  kuelezea  uhalisi  wake,  kuiambia  dunia  nzima  kwamba  kuzimu  ni  halisi,  na
kuwatoa waliopotea kutoka gizani kuingia kwenye nuru ya injili ya Yesu Kristo
.
Mara ile ile, roho yangu ilitolewa ndani ya mwili. Nilitoka na Yesu kutoka  ndani ya chumba
changu  tukaingia  hewani.  Nilikuwa  na  ufahamu  wa  mambo  yote  yaliyokuwa
yananizunguka. Nilimuona mume wangu na watoto wamelala pale chini nyumbani.
Ilikuwa  kama  nimekufa  na  mwili  wangu  umeachwa  nyuma  kwenye  kitanda  wakati  roho
yangu inapanda juu na Yesu kupitia paa la nyumba. Ilikuwa kama paa lote limeezuliwa, na
niliona familia yangu imelala vitandani.
Niliona  Yesu  akinigusa  na  kuniambia,
Usiogope.  Watakuwa  salama
.
Alitambua
mawazo yangu.
Nitajihidi kwa kadri ya uwezo wangu kueleza hatua kwa hatua niliyoyaona na nilivyojisikia.
Mambo  mengine  sikuelewa.  Bwana  Yesu  alinieleza  maana  ya  mambo  mengi,  lakini
mambo mengine hakuniambia.
Nilifahamu  wakati  ule,  na  sasa  nafahamu,  kwamba  mambo  haya  yalikuwa  yanatokea
kihalisi na Mungu mwenyewe ndiye  angeweza kunionyesha. Litukuzwe Jina lake.  Jamani,
niamini, kuzimu ni  halisi.Nilipelekwa  kule na  Roho  mara  nyingi  wakati wa kuandaa taarifa
hii.
Mara tulikuwa katika anga za juu. Niligeuka na kumtazama Yesu. Alikuwa amejaa utukufu
na nguvu,  na amani ya ajabu ilifurika kutoka kwake. Alichukua  mkono wangu na kusema,
Nakupenda. Usiogope, maana niko pamoja nawe
.”
Baada  ya    hayo,  tulianza  kupaa  juu  zaidi  mawinguni,  na  sasa niliweza  kuiona  dunia  kwa
chini.  Katika  sehemu  nyingi  kulikuwa  na  mashimo  (faneli)  yaliyokuwa  yanajizungusha
kueleka mahali fulani,  na kurudi tena  yalikotoka.. Haya  yalikuwa yanatembea  juu sana  ya
dunia na  yalikuwa  kama kitu fulani kikubwa,  kichafu  na kinachoteleza kinazunguka wakati
wote.    Vilikuwa  vinajitokeza  duniani  pote
".vitu  gani  hivi?”
Nilimuuliza  Bwana  Yesu
tulipokuwa tunakikaribia kimojawapo.
"
Haya ni malango ya kuzimu,
Aliniambia.
Tutaingia kwenye mojawapo
.
Mara tuliingia mojawapo ya mashimo haya. Ndani lilionekana kama tanuru, likizunguka na
kuzunguka kama pia.
Giza  nene  ilituangukia,  na  pamoja  na  giza  hilo  ilikuja  harufu  mbaya  sana  kiasi  cha
kwamba ilikausha pumzi yangu. Kwenye kuta
za shimo hili kulikuwa na viumbe vimeganda
kwenye  kuta.  Vilikuwa  na  rangi  ya  zambarau,    viumbe  hivi  vilitembea  na  kupiga  kelele
tulipopita.  Nilijua bila kuambiwa kwamba vilikuwa viovu.
Viumbe hivi vingeweza kutembea lakini viliganda kwenye kuta. Vilitoa harufu mbaya sana,
na  vilitupigia  kelele  zenye  kukera  kweli.  Nilihisi  nguvu  fulani  ya  giza,  isiyoonekana,
ikitembea ndani ya mapango.
Wakati  fulani, katika giza, niliweza kuona  maumbile. Chura mchafu  alijaza kuta za  pango.
Bwana vitu gani hivi
?” Niliuliza huku nikishika mkono wa Yesu kwa nguvu.
Alisema,  "
Hizi  ni  roho  chafu  ambazo  ziko  tayari  kumwagwa  duniani  pindi  Shetani
atakapotoa amri
.
"
Tulipokuwa  tunashuka  kwenye  pango,  viumbe  hivyo  viovu  vilicheka  na  kutuita.  Vilijaribu
kutugusa, lakini havikuweza kwa sababu ya nguvu ya Yesu. Hewa yenyewe ilikuwa chafu,
ni uwepo wa Yesu tu ulionizuia kupiga kelele kwa utisho mkubwa uliokuwepo
.Oh,  ndio,  nilikuwa  na  fahamu  zangu  zote
niliweza  kusikia,  kunusa,  kuona,  kugusa  na
hata  kuonja  uovu  wa  mahali  hapa.  Zaidi  ya  hapo  fahamu  zangu  zilikuwa  makini  zaidi,
harufu na uchafu vilinitia kichefuchefu.
Mayowe  yalijaza  hewa  tulipokaribia  mwanzo  wa  shimo.  Vilio  vikali  vilipanda  juu  na
kutulaki. Sauti za kila namna ziliijaza hewa. Nilisikia hofu, mauti na dhambi vikinizunguka.
Harufu  mbaya  ambayo  sijawahi  kunusa  iliijaza  hewa.  Ilikuwa  harufu  ya  mzoga  unaooza,
na ilielekea kutoka kila upande. Kamwe hapa duniani nilikuwa sijawahi kuhisi kiasi hiki cha
ouvu  au  kusikia  sauti  za  namna  hii  za  kukata  tamaa.  Muda  si  muda  ningeligundua
kwamba mayowe haya yalikuwa ya wafu na kwamba kuzimu kulijaa mayowe yao.
Nilisikia  mvumo  wa  upepo  mbaya  na  mvuto  mdogo  mbele  yetu.  Mwanga  kama  wa  radi
ulipenyeza kwenye giza nene na kutupa vivuli vyeusi  vyeusi kwenye kuta.  Niliweza kuona
umbile  la  kitu  fulani  mbele  yangu.  Nililishtuka  nilipotambua  kwamba  joka  kubwa  lilikuwa
linatambaa  mbele  yetu.  Nilipoendelea  kutazama  niliona  nyoka  wengi  wabaya
wanatambaa kila mahali.
Yesu aliniambia "
Muda si mrefu tutaingia kwenye mguu wa kushoto wa kuzimu. Huko
mbele  utaona  huzuni  kubwa,  masikitiko  ya  kutisha  na  vitisho  visivyoelezeka.  Kaa
karibu na  Mimi,  nami  nitakupa  nguvu  na  ulinzi  tunapopita kuzimu.  Mambo  ambayo
utayaona  ni  tahadhari,
Aliniambia.
"
Kitabu  utakachokiandika    kitaziokoa  roho
nyingi  zisiende  kuzimu.  Unayoyaona  ni  halisi.  Usiogope,  kwa  maana  nitakuwa
pamoja nawe
Hatimaye,  Bwana  Yesu  namimi  tulifika  chini  ya  shimo.  Tuliingia  kuzimu.  Nitajitahidi  kwa
uwezo  wangu  wote  kukueleza  niliyoyaona,  na  nitasimulia  kwa  ule  mpangilio  ambao
Mungu alinipa.
Mbele yetu, kwa kadri nilivyoweza kuona, kulikuwa na vitu vinaruka huku na kule. Sauti za
kukoroma  na  vilio  vya  huzuni  viliijaza  hewa.  Juu  niliona  mwanga  hafifu,  na  tulianza
kuufuata. Njia  ilikuwa kavu na  yenye  mavumbi.  Mara  tulifika kwenye mlango wa  kuelekea
kwenye shimo dogo lenye giza.
Mambo  mengine  siwezi kuyaandika  kwenye karatasi;  yalikuwa yanatisha  mno kuyaeleza.
Kuzimu  hofu unaisikia hasa,  na  nilijua  kwamba kama nisingelikuwa  na Yesu  nisingeweza
kurudi.  Katika  kuandika  haya,  baadhi  ya  mambo  niliyoyaona  sikuyaelewa,  lakini  Bwana
anajua yote, na alinisaidia kuelewa mambo mengi niliyoyona.
Nakuonya,  usiende  mahali  kule.  Ni  mahali  penye  mateso  ya  ajabu,  maumivu  makubwa,
na  huzuni  ya  milele.  Roho  yako  itakuwa  hai  wakati  wote.  Roho  inaishi  milele.Roho  ndio
wewe, na roho yako itakwenda mbinguni au kuzimu.
Kwa  wale  mnaodhani  kwamba  kuzimu  ipo  hapa  duniani
sawa,  ipo  hapa.  Kuzimu  ipo
katikati  ya  dunia,  na  kule  kuna  roho  ziko  kwenye  mateso  usiku  na  mchana.  Kuzimu
hakuna  sherehe. Hakuna upendo, hakuna kuhurumiana. Hakuna kupumzika. Ila ni mahali
penye masikitiko zaidi ya unavyoweza kudhani.

MUNGU NA AKUBARIKI TUKUTANE SEHEMU YA PILI.....