Nov 5, 2014

MAISHA NI KUCHAGUA

      Mara kwa mara imetokea pindi unapojikuta njia panda, ukiangalia ni kama dunia yote imegeuka kuwa debe la misumari ambayo imeishakutoboatoboa na kukuchuna kiasi ambacho haufahamiki tena wewe ni nani katika ulimwengu huu.
      Siku za nyuma ulikuwa na maono makubwa sana, ulijiamini na ulijua hakuna kinachoweza kukushinda, mara nyingi ulitumia muda wako kwa shughuli za maendeleo lakini  sasa hivi unaona kama dunia sio yako tena.
      Ningependa nikwambie kwamba usistushwe na hali uliyonayo kwa sasa, maana kila kunapokucha ni darasa jipya na ukurasa mpya katika maisha yako, ni vema ukachukua muda mpya kuziamgalia nafasi mpya zilizopo katika eneo lako. Katika ulimwengu huu unaobadilika badilika kutokana na maendeleo ya kiteknolojia ni lazima na wewe ubadilike ili uweze kuendana nao, hii itakusaidia hasa kujijua upo katika wakati gani, na nini ufanye ili uweze kuondokana na hali mbaya inayokuzunguka!

Nini ufanye basi,
             chukua muda wako mwingi katika kujisomea vitabu vya mafundisho ya namna mbalimbali, vitabu hivi vinaweza kuwa vya mafundisho ya ujasiliamali, mafundisho ya KIMUNGU, shuhuda za kawaida na KIMUNGU na vinginevyo madamu visiwe vya mambo ya kufikirika, hivi vitakusaidia kuchangamsha ufahamu wako na kuona wengine wametoka wpi na wanenda wapi na wewe upo wapi hasa.
         Kitu kingine jitahidi uwe mtu wa kuutumia mtandao kwa manufaa ya kujiendeleza, unajua kwenye mtandao kuna kila kitu, ni kama kuwa baharini kuna samaki waliwao naa wasioliwa, ni jukumu la mvuvi kujua achue samaki wa namna gani, basi hata wewe unapopata fursa ya kuwa usipende kwenda kurasa zisizokuwa na manufaa katika maisha yako, badala yake jifunze kutafuta vitu vitakavyokuletea maendeleo!
         Jambo lingine jitahidi kupunguza marafiki wasiokuwa na maana katika maisha yako, maana wengi wao wanakupotezea muda wako mwingi na wengine ndio sababu ya wewe kuwa hapo ulipo, tambua kuwa mtu mwenye uwezo wa kuyafanya maisha yako kuwa bora au mabaya ni wewe mwenyewe hivyo usije jikuta unabaki kumlaumu mtu flani wakati ni wewe ambaye ulimpa nafasi katika maisha yako.

SIKU ZOTE TAMBUA MAISHA NI MFURULIZO WA MACHAGUZI, HIVYO JITAHIDI KUFANYA UCHAGUZI MWEMA.

 

No comments:

Post a Comment